Wakati hatima ya Louis Van Gaal ikiwa haieleweki Klabuni
Manchester United msimu ujao, Mourinho amekuwa akihusishwa sana na kuchukua
mikoba ya Mholanzi huyo aliyebakiza mwaka mmoja klabuni hapo.
Mourinho ametokea kuwa mtu anaejadiliwa sana linapokuja
suala la nani atarithi mikoba ya Van Gaal.
Kufika kwa Mourinho Chelsea kulipelekea Mata kuuzwa kutoka
Chelsea na kwenda Man United Januari 2014. Hata hivyo Mhispania Mata hakupenda
ku-comment chochote pale alipotakiwa kuzungumzia tetesi za ujio wa Mourihno Man United.
Mata aliiambia Daily Mail kuwa “Sidhani kama itakuwa sahihi
kulizungumzia hili suala kwa sasa wakati ambapo tunae Kocha tayari, na tuna
vitu vya msingi zaidi mbele yetu vya kuvifanya katika msimu huu”.
“Sio wakati sahihi kuzungumzia suala hilo” aliongeza Juan
Mata ambae aliuzwa na Mourinho kutoka Chelsea.
Mata leo anatarajiwa kuungana na wachezaji wenzie kuzisaka
pointi tatu ili ziwasogeze karibu na top 4 ambapo wataweza kushiriki mashindano
ya UEFA Champions League msimu ujao.
Pata habari za michezo kwa haraka zaidi kupitia soka24.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment