Sunday, May 1, 2016

MAN UNITED WACHELEWESHA SHEREHE ZA UBINGWA LEICESTER CITY


LEICESTER City walikaribishwa katika dimba la Old Trafford kutafuta pointi 3 ambazo zilikuwa zinawatosha kuwa mabingwa wapya wa ligi kuu nchini Uingereza. Lakini tofauti na ilivyosubiriwa na wengi kwamba huenda Leicester wangezitwaa pointi 3 hizo Old Trafford kwa kile kilichoonekana kiwango kibovu cha siku za hivi karibuni kinachoonyeshwa na Man United, Leo hali imekuwa tofauti baada ya Mashetani wekundu hao kuwalazimisha sare ya 1 - 1 vijana wa Mzee Ranieri.
Antonio Martial ndiye alikuwa wa kwanza kuifungia Man United goli la kwanza dakika ya 8 akiunganisha mpira wa krosi, Leicester hawakukata tamaa licha ya kuwa walikuwa wakicheza kwa presha kubwa na mnamo dakika ya 17, Morgan aliisawazishia goli Leicester na kufanya matokea kuwa 1 - 1. Man United walilishambulia sana lango la Leicester lakini vijana hao wa Claudio walipambana kweli kweli kuhakikisha wanaitunza hata hiyo pointi moja waliyoipata. 
Hadi mchezo huo unamalizika Matokeo ni Man United 1 - 1 Leicester, hivyo kuwafanya Leicester kusubiri game ijayo dhidi ya  ambapo wakishinda basi watakuwa mabingwa wapya wa EPL msimu wa 2015/2016.
kwa sasa Leicester wamefikisha pointi 77 wakiwa wamecheza michezo 36 katika nafasi ya kwanza, Man United nao wamefikisha pointi 60 katika nafasi ya 5 kwa michezo 35 waliyocheza.




Pata habari za michezo kwa haraka zaidi kupitia soka24.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment