MECHI ya Ligi kuu Bara kati ya Simba na Azam Fc imemalizika kwa timu hizo kutoka suluhu ya 0 - 0, Mchezo ulikuwa wa taratibu sana kipindi cha kwanza lakini kipindi cha pili hasa baada ya vurugu zilizotokea baada ya mchezaji wa Azam kumkanyaga kwa makusudi Hamisi Kiiza, timu ziliongeza kasi na kushuhudia mashambulizi ya mara kwa mara katika pande zote mbili.
Matokeo haya yamepokelewa kwa furaha kwa upande wa Yanga kwani kwa sasa gepu kati yao na timu hizo linaongezeka na kufikia pointi 6 kwa Azam Fc na pointi 7 kwa upande wa Simba, Hivyo Yanga inatakiwa kushinda Mechi 2 tu kati ya 4 zilizobaki ili kuwa mabingwa kwa mara ya pili mfululizo.
Pata habari za michezo kwa haraka zaidi kupitia soka24.blogspot.com
Pata habari za michezo kwa haraka zaidi kupitia soka24.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment