Mshahara huo ni mdogo zaidi ukilinganisha na ule anoupata Andy Carroll anayeitumikia Klabu ya West Ham United na ni nusu ya Mshahara anaoupata Bacary Sagna wa Manchester City.
Ukata wa Star huyo wa Barcelona ndio sababu ya vilabu vingi vya Ligi ya Uingereza kutaka kumsajili kutokana na kiwango chake bora alichokuwa nacho kisichoendana na kipato anachokipata. Lakini Mbaya zaidi katika Mtandao wa Daily Mail unaonyesha kwamba kwa timu yoyote itakayo taka kumsajili italazimika kutoka kitita cha paun za Kiingereza Milioni 150, thamani ambayo ni kubwa zaidi kwa vilabu kuweza kufikiria kumsajili Mbrazili huyo, kwahiyo kama hakuna klabu itayojitokeza kutoa dau hilo nono Neymar ataendelea kutumikia Barcelona akilipwa Mshahara huo ambao unaonekana ni mdogo sana ikilinganisha na kiwango bora alichokuwa nacho mchezaji huyo.
Zlatan Ibrahimovic ambae kamwe hawezi kukubali kulipwa pesa ndogo kama ilivyo kwa Neymar anahusishwa na kujiunga na Manchester United licha ya Vilabu vya Arsenal, Chelsea, Liverpool na China kuonesha nia ya kutaka kumsajili.
0 comments:
Post a Comment