Tuesday, April 12, 2016

Beki Kisiki Wa Manchester City Nje Tena Leo Dhidi Ya PSG


Nahodha wa Manchester City Vicent Kompany atakosa tena mechi ya robo fainali klabu bingwa Ulaya maarufu kama UEFA Champions League leo  katika uwanja wa Etihad dhidi ya PSG.

"Hayuko fiti 100%, haiwezekani Kumchezesha" Alisema Manuel Pelegrini Meneja wa Manchester City.

Kompany (30), Hajawahi kucheza mechi yoyote tangu kuumia kwake katika mchezo dhidi ya Dynamo Kiev mwezi Machi  mchezo ambao uliisha kwa suluhu ya 0 - 0. City na PSG wanakutana ikiwa ni marudiano ya mchezo wa kwanza uliochezwa nchini Ufaransa na kushuhudia timu hizo zikitoka sare ya 2 - 2.

Kompany amekuwa akiandamwa na majeruhi siku za hivi karibu kitu ambacho kinaifanya Man City kusuasua katika eneo lake la ulinzi.

0 comments:

Post a Comment