Tuesday, April 12, 2016

LIVE Droo Ya Nusu Fainali Kombe La Shirikisho ASFC Leo


Droo ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup), inatarajiwa kufanyika leo Jumanne saa 3 usiku moja kwa moja (live) kupitia kituo cha luninga cha AzamTwo.

Hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho (ASFC) itafanyika live katika kituo cha AzamTwo, ambao kupitia Azamtv ndio wadhamini wa wakuu wa michuano hiyo iliyoibua msisimiko wa mpira wa miguu na kushirikisha timu nyingi zaidi nchini.

Michuano ya Kombe la Shirikisho iliyoanza kwa kushirikisha timu 64 mwishoni mwa mwaka jana, imefikia hatua ya nusu fainali, baada ya Azam FC kuindoa Prisons (3-1), Mwadui FC kuiondosha Geita Gold (3-0) na Yanga SC kuwaondoa Ndanda FC kwa mabao (2-1) na jana Coastal Union Kuwaondoa Simba (1-2).

Mshindi wa Kombe la Shirikisho (ASFC) msimu huu, ataiwakilisha Tanzania mwaka 2017 katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF CC).

0 comments:

Post a Comment