Tuesday, April 12, 2016
Yanga Na Mwadui, Azam FC Na Mtibwa
Michuano ya Ligi kuu Tanzania Bara maarufu kama Vodacom Premier League ( VPL ) inatarajiwa kuendelea tena hapo kesho kwa mechi mbili.
Yanga iliyotoka kumenyana na Al Ahly juzi itawakaribisha vijana wa Jamhuri Kiwelu Julio katika Uwanja wa taifa kesho Jumatano, Mechi nyingine itahusisha timu za Azam Fc na Mtibwa kutoka Jijini Morogoro. Azam Fc watasafiri kuifuata Mtibwa Wakati Yanga wakiwa taifa kuisubiri Mwadui Fc.
Yanga ambayo inashika nafasi ya pili katika Msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 53 ikiwa imeshacheza michezo 22 michezo miwili nyuma ya Simba SC inayoshika nafasi ya kwanza kwa pointi 57 ikiwa imekwishacheza michezo 24, inahitaji Ushindi ili iweze kuchuana na timu za Simba na Azam katika mbio za kumtafuta bingwa wa Ligi kuu Msimu huu.
Azam wao wapo katika nafasi ya 3 wakiwa wamejikusanyia pointi 52 katika michezo 23 waliyocheza.
Mwadui iliyopo chini ya Kocha mwenye maneno mengi Jamhuri Kiwelu Julio inashika nafasi ya 6 ikiwa na pointi 34 katika michezo 25, Mtibwa nao wapo katika nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi wakiwa wamekwishacheza Mechi 24 na pointi zao 43.
Mechi hizo ni muhimu kwa timu zote ila ni muhimu zaidi kwa Azam na Yanga ambao wanagombea nafasi ya Ubingwa wa ligi Msimu huu wa 2015/2016.
0 comments:
Post a Comment