BEKI kisiki wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Shomari Kapombe, anaendelea vema na matibabu nchini Afrika Kusini huku ikielezwa kuwa afya yake inazidi kuimarika kadiri siku zinavyosogea.
Kapombe yupo jijini Johannesburg nchini humo katika Hospitali ya Morningside Mediclinic tokea Alhamisi iliyopita akipatiwa matibabu baada ya kugundulika na ugonjwa wa Pulmonary Embolism (donge la damu kuziba mishipa ya damu katika mapafu).
Akizungumza na mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz Daktari wa timu ya Azam FC, Dr. Juma Mwimbe, alisema kuwa kwa mujibu wa taarifa alizopata leo kutoka huku ni kuzidi kuimarika kwa afya ya beki huyo.
“Tunamshukuru Mwenyenzi Mungu anaendelea vizuri sana, nimeongea naye leo asubuhi na ameniambia anajisikia vizuri sana na maumivu kwenye kifua yamepungua na kubakia kwa umbali sana, mpaka sasa hatujajua atarejea lini nchini kwani bado anaendelea na matibabu,” alisema.
Mwimbe alisema Kapombe anahitaji mapumziko ya miezi miwili hadi mitatu ili kuweza kurejea katika hali yake ya kawaida, hivyo atazikosa mechi zote zilizobakia za Azam FC msimu huu na huenda akarejea uwanjani kwenye kipindi cha maandalizi ya msimu ujao.
Beki huyo wa zamani wa Simba na AS Cannes ya Ufaransa, amekuwa na kiwango kizuri msimu huu kwani mpaka sasa ameshaifungia Azam FC mabao 11, nane kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), mawili Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) na moja amefunga ndani ya Kombe la Shirikisho Afrika (CC) wakati timu hiyo ikiilaza Bidvest Wits mabao 3-0.
chanzo: Azamfc Official site
soka24 Inaungana Na Watanzania Wote Katika Kumuombea Kapombe Apone Haraka
Tuesday, April 12, 2016
Afya Ya Kapombe Yazidi Kuimarika
Related Posts:
MSAFARA WA YANGA WAWASILI SALAMA JIJINI DAR Hapa Timu Ikielekea Makao Makuu Baada Ya kutua katika uwanja wa ndege wa Mwalimu JK Nyerere … Read More
MASHABIKI WAFURIKA UWANJA WA NDEGE KUISUBIRI YANGA Msafara wa klabu ya Yanga unatarajia kuwasili Leo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Mashabiki wakiwa wanawasubiri kwa hamu kubwa mashujaa wao waliotinga hatua ya robo fainali … Read More
YANGA; "KOMBE LA UBINGWA LIGI KUU HALINA HADHI" Ofisa habari wa klabu ya Yanga Jerry Muro amelikosoa kombe la ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara kwa kusema halina Hadhi. Akizungumza na waandishi wa Habari jana Muro alisema kombe hilo halina hadhi ukilinganisha na uku… Read More
SHABIKI MKUBWA WA YANGA AUAWA KWA KUPIGWA RISASI Shabiki Mkubwa Wa Yanga Askari Wa Jeshi La Polisi Kikosi Cha Usalama Barabarani Kinyogori Ameuawa Kwa kupigwa Risasi. Kinyogoli Enzi Za Uhai Wake Askari wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Sajini Kinyogor… Read More
SALUM MAYANGA HUYU NI CLAUDIO RANIERI WA LIGI KUU BARA Kutoka Katika kupigania kutoshuka Daraja Msimu wa 2014/15 Hadi Kushika Nafasi Ya 4 Katika Ligi Kuu Tanzania Bara Msimu Wa 2015/16, Ni Dhahiri kuwa Mayanga Ni Bonge La Kocha. Salum Mayanga Itakumbukwa kuwa msimu wa 201… Read More
0 comments:
Post a Comment