Tuesday, April 12, 2016

Adam Johnson Kukata Rufaa

Mchezaji Adam Johnson amefikia maamuzi ya kukata rufaa kufuatia sakata lake la kufanya mapenzi na binti mwenye umri wa chini ya miaka 18, Johnson ameamua kufikia maamuzi hayo baada ya hukumu yake ya kifungo cha miaka sita jela aliyoipata hivi karibuni.

Adam ambae pia kibarua chake kilioteshwa nyasi katika klabu ya Sunderland kufuatia kashfa hiyo alihukumiwa miaka sita jela mwezi uliopita katika mahakama ya Bradford Crown  baada ya Hakimu Jonathan Rose kusema Johnson amemsababishia binti huyo matatizo makubwa ya Kisaikolojia.

Johnson (  28 ) Mchezaji wa zamani wa Middlesbrough na Manchester City tayari ameshapeleka rufaa yake kupinga hukumu hiyo inayomhusisha na kutenda tendo la ndoa na binti mwenye umri wa miaka 15 kwa kukusudia, shitaka ambalo awali alipatikana na hatia.
Dada wa mchezaji huyo anejulikana kwa jina la Faye ambae ndo anafatilia rufaa ya ndugu yake akiwa pia ameanzisha ukurasa maalumu wa facebook unaoitwa “Adam Johnson’s Appeal Fight” alinukuliwa akisema “Rufaa ya Adam kupinga hukumu yake tayari imeshapelekwa”, “Shukrani kwa kila mtu kwa msaada wenu Munaotuonyesha, hiyo inamaana kubwa sana kwetu” aliongezea Faye.

Ukurasa huo wa Adam Johnson’s Appeal Fight hadi sasa umeshapata likes zaidi ya 8,000.


Katika shitaka hilo la aibu la Adam Mahakama ilionyeshwa jinsi Adam alivyokuwa akitumiana meseji na Binti huyo  ambazo zilikuwa zinamshawishi binti huyo azifute meseji zote ambazo Adam alikuwa akimtumia ili kufuta ushahidi. Adam alikiri kukutana na binti huyo kwenye gari lake aina ya Range Rover januari 30 mwaka jana na kumkisi tu basi binti huyo kwenye gari. Lakini msichana huyo aliiambia mahakama kuwa Johnson hakuishia tu katika kumkisi bali alienda mbali zaidi na hatimaye Johnson akapatikana na hatia.

0 comments:

Post a Comment