Tuesday, April 12, 2016

"Mapema Sana Kumwita Van Gaal Failure" Jordi Cruyff

Van Gaal

Nyota wa Zamani wa Barcelona na Manchester United Jord Cruyff amewabeza wanaomponda kocha wa Manchester United Louis Van Gaal kwa kuwaambia ni mapema sana kumwona kocha huyo ni failure (aliefeli ). Jord aliongea maneno hayo yanayoonyesha kumkingia kifua Louis Van Gaal anaeonekana kuwa si chochote mbele ya Mashabiki kutokana na mwenendo wa timu hiyo kwa sasa.

“Louis Van Gaal anahitaji kupewa muda zaidi Man United”  yalikuwa ni maneno ya Jordi Cruyff.
Tetesi za kocha wa zamani wa Chelsea Jose Mourihno kujiunga na Man United kuchukua nafasi ya Van Gaal Msimu wa 2016/2017 Cruyff anaona sio kitu sahihi kwa sasa
.
Jordi Cruyff Nyota Wa Zamani Wa Man U
“Nafikiri neno kufeli linamaana kubwa sana” alisema Jordi akiiambia Omnisport machi 18 mwaka huu. “kuna mechi nyingi bado za kucheza, kama wakiishia kushinda kombe la FA na kumaliza katika nafasi ya pili katika ligi sidhani kama watu wataona huko ni kufeli, wataona hiyo ni kama kujiimarisha” aliongeza Cruyff.

“Itakuwa ni kitendo cha kikatili na cha haraka sana kumfukuza kwa sasa, japo ni wazi kuwa mambo hayaendi  sawa kama ambavyo wengi walitarajia licha ya uwekezaji mkubwa uliofanyika klabuni hapo” alisema Cruyff.


Man United ipo katika kipindi kigumu kwa sasa kufuatia vichapo inavyopokea kutoka kwa timu pinzani pia ikiwa haina uhakika wa kushiriki michuano ya UEFA msimu ujao. Mchezo wao wa mwisho waliocheza na Tottenham walikubali kichapo cha magoli matatu kwa bila na Wanatarajia kucheza na West Ham United Jumatano hii katika Uwanja wa Upton Park.

0 comments:

Post a Comment