Sunday, April 24, 2016
Home »
Kimataifa
,
Laliga
» Zinedine Zidane Akwepa Uvumi Unaomhusisha James Rodriguez Kuondoka Madrid
Zinedine Zidane Akwepa Uvumi Unaomhusisha James Rodriguez Kuondoka Madrid
kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane amekwepa kutolea maelezo uvumi unaosambaa kuhusu mchezaji wake James Rodriguez kuihama klabu hiyo.
James amekuwa akisugua benchi siku za hivi karibuni hali ambayo inazua mijadala kwa wapenzi wa mchezaji huyo. katika mchezo wa jana dhidi ya Rayo Vallecano James alitokea benchi Madrid ikishinda kwa magoli 3 - 2.
"sioni tatizo lolote kwa James, ni mchezaji mzuri na ni mchezaji muhimu pia kwa klabu, alicheza vizuri na alifunga goli katika mchezo wetu dhidi ya Eibar na Getafe. Na anahitaji kucheza mechi nyingi zaidi, lakini hali hiyo inamkuta kila mchezaji ambae huwa hajacheza kwa muda mrefu. Nina wachezaji 24 katika kikosi changu na nahitaji kuwachagua 11 tu kati ya hao, muda mwingine inaonekana kama nahitaji kufanya mabadiliko matatu katika kila mchezo, lakini nitafanya hivyo endapo tu nitaona ulazima wa kufanya hivyo, mimi ndio kocha na ndio nafanya maamuzi" alisema Zidane
Inasemekana James alikuwa na mahusiano mazuri sana na Kocha Rafael lakini tangu kuja kwa Zidane muda mwingi amekuwa akikaa benchi na katika mechi 8 za hivi karibuni za Real Madrid, James ameanza kikosi cha kwanza katika mechi mbili tu.Hali hii ndo inayoleta uvumi wa kwamba huenda Mkolombia huyo akaondoka klabuni hapo.
pata habari za michezo kwa haraka zaidi kupitia soka24.blogspot.com
Related Posts:
FERGUSON: Ronaldo na Messi, wakizeeka Soka la hispania litadorora Kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson anaamini soka la Hispania litakoma kutawala ulaya katika ngazi ya vilabu. Katika kipindi cha miaka nane iliyopita vilabu vya Hispania vimetwaa kombe la ligi ya mabi… Read More
Laliga: michezo kadhaa kupigwa leo hii, Barcelona vs Sporting Gijon Barcelona vs Sporting Gijon 21:30 Celta Vigo vs Espanyol 21:30 Osasuna vs Villarreal 21:30 Granada vs … Read More
Msimamo wa Laliga Baada ya mechi za jana jumamosi february 18 Matokeo ya jana raundi ya 23 na msimamo wa ligi kuu ya Hispania ni kama ifuatavyo: Sporting Gijon 1 - 4 Atletico Madrid Real Madrid 2 - 0 Espanyol Deportivo La Coruna 0 - 1 Alaves Sevilla 2 - 0 Eibar… Read More
Atletico Madrid 1 - 2 Barcelona, messi aipeleka Barcelona kileleni Timu ya Barcelona imetambatia timu ya Atletico Madrid baada ya kuichapa goli 2 - 1. Mpira ulianza kwa kasi kila timu ikifika langoni mwa mpinzani, 4' Diego Godin alikosa goli la wazi. mpira uliendelea kuwa wa ko… Read More
Atletico Madrid vs Barcelona kumbukumbu muhimu kabla ya mchezo wao wa leoMUDA: 18:15 UWANJA: Estadio Vicente Calderon REFARII: Antonio Mateu (Spain) Kuelekea kwenye mchezo mkubwa wa mwisho wa wiki tunakuletea tathimini fupi… Read More
0 comments:
Post a Comment