Sunday, April 24, 2016

Tetesi Zinaonyesha Kuwa Star Huyu Wa Man Utd Atajiunga Na Real Madrid


Uwezekano wa kipa namba moja wa Man Utd David De Gea kujiunga na Real Madrid katika msimu ujao wa usajili unazidi kuongezeka baada ya kapteni wa Madrid Sergei Ramos kuzungumza katika vyombo vya habaari hivi karibuni akisisitiza kwamba ni wazi kuwa mlinda mlango huyo atajiunga na wababe hao wa ligi ya Hispania.

Mhispania huyo mwenye miaka 25 alijiunga na mashetani wekundu mwaka 2011 akitokea katika klabu ya  Atletico Madrid kwa kitita cha paundi milioni 17. De Gea alishahusishwa na kujiunga na vigogo hao wa Hispania msimu uliopita hata hivyo aliongeza mkataba na Man Utd baada ya dili lake la kujiunga na Madrid kufeli katika dakika za mwisho kutokana na kutofikia muafaka kati ya klabu hizo mbili juu ya mchezaji huyo.

Uvumi unaoenea kwa kasi hivi sasa ni kuwa itakuwa ni ndoto kubwa iliyotimia kwa De Gea kujiunga na Madrid licha ya kuwa mlinda mlango huyo anaonekana kuwa na furaha katika klabu hiyo kwa sasa. Ramos aliendelea kwa kusema “ kama viongozi wa juu wa timu ( Real Madrid) wenyewe wanaamini De Gea ni Golikipa bora na wao mahitaji yao ni kuwasainisha wachezaji bora, basi ni wazi De Gea lazima atakuja Madrid”

Ukweli wa tetesi hizi utategemea tu nani atalishikilia jambo hili katika klabu ya Man Utd msimu ujao, haijulikani kama Jose Mournho anaweza kumruhusu mchezaji huyo kuondoka klabuni hapo.

Related Posts:

  • FARID MUSSA ASUBIRI RUHUSA YA AZAM FCFarid Mussa ni winga wa Azam FC aliyepata nafasi ya kwenda kufanya majaribio katika klabu ya Deportivo Tenerife ya nchini Hispania na kufanikiwa kufuzu majaribio hayo na sasa anasubiri ruhusa ya klabu tu ili aondoke zake. … Read More
  • SHOMARI KAPOMBE KURUDI MSIMBAZIKlabu ya Simba imesema inapambana kuhakikisha wanamrudisha kikosini beki wao Shomari Kapombe anayeitumikia klabu ya Azam FC kwa sasa. Kapombe ambaye hivi karibuni ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa msimu uliopita ligi kuu Vo… Read More
  • NONGA AOMBA VILABU VIJITOKEZE KUMSAJILIPaul Nonga ameziomba klabu ambazo zinahitaji huduma yake kufanya mazungumzo na Yanga. Mshambuliaji huyo ambae hivi karibuni aliuandika uongozi wa Yanga barua akiwa anaomba umuuze kwenye timu nyingine kutokana na kuchoshwa … Read More
  • SIMBA YANASA KIFAA KINGINE KIPYAKlabu ya Simba imempa mkataba wa miaka miwili kiungo Mohamed Ibrahimu tayari kwa kuitumikia klabu hiyo msimu ujao. Rais wa Simba ameyathibitisha hayo kwa kusema usajili wa Ibrahimu utasaidia kuimarisha timu yao ambayo ina … Read More
  • MIPANGO YA JULIO KATIKA USAJILIKocha wa Mwadui FC, Jamhuri Kiwelu "Julio" amesema yeye hana mpango wa kusajili wachezaji wa kigeni katika kikosi chake. Julio amesema lengo lake ni kutoa fursa kwa wachezaji wa ndani waweze kuonyesha uwezo wao ili waje ku… Read More

0 comments:

Post a Comment