Sunday, April 24, 2016

MATCH PREVIEW: Coastal Union vs Yanga


kombe la shirikisho Azam Sports Confederation Cup linaendelea tena leo katika hatua ya nusu fainali ambapo katika uwanja wa mkwakwani huko jijini Tanga, Wenyeji Coastal Union wanawakaribisha Vijana wa jangwani Dar Young Africans.

Coastal ambao wameingia katika hatua hiyo baada ya kuwatoa Simba katika mchezo wa robo fainali uliochezwa katika uwanja wa taifa kwa ushindi wa bao 1 - 0 ilipangwa na Yanga baada ya droo iliyofanyika siku chache zilizopita.

Coastal Union wanahitaji kufuzu hatua hii na kuweza kucheza hatua ya fainali na ikiwezekana kuchukua ubingwa ili waweze kushiriki katika mashindano ya shirikisho CAF, kwani mwenendo wao katika ligi bado ni wa kusuasua. Coastal inashika nafasi ya mwisho katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 22 katika mechi 27 walizocheza hadi hivi sasa, lakini kwa mechi za hivi karibuni wamekuwa wakifanya vizuri.

Nao Yanga wanahitaji ushindi leo katika dimba hilo la mkwakwani ili wajihakikishie kucheza hatua ya fainali ya kombe hilo na hata kuchukua ubingwa kutokana pia na ushindani mkubwa uliopo katika ligi kuu. Yanga inashika nafasi ya kwanza kwa pointi 59 ikiwa imecheza mechi 24 ikifuatiwa na Simba wenye pointi 57 katika mechi 24 walizocheza huku Azam wakishika nafasi ya 3 kwa pointi 55 katika michezo 24 waliyocheza. 

Yanga imeingia katika hatua ya nusu fainali baada ya kuiondosha Ndanda FC kutoka Mtwara kwa jumla ya magoli 2 - 1.

Yanga ambayo imetokea nchini Misri ambako walienda kucheza mashindano ya klabu bingwa Afrika na Al Ahly itaingia uwanjani ikikumbuka kichapo cha goli 2 - 1 ilichopokea kutoka kwa waarabu hao wa Misri.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa ni wa ushindani mkubwa kutokana na upinzani mkali uliopo kati ya klabu hizo mbili.

Ungana na Soka24 kufuatilia mechi hiyo kwa kila litakalojiri katika mchezo huo huko jijini Tanga,

0 comments:

Post a Comment