Thursday, May 12, 2016

KUMBE HUYU NDO ALIYEIFUNGISHA MAN UTD DHIDI YA WESH HAM


Manchester United ilishindwa kupata ushindi waliokuwa wanauhitaji ili wajihakikishie nafasi ya nne katika msimamo wa ligi kuu nchi Uingereza baada ya kukubali kipigo cha 3 – 2 kutoka kwa wagonga nyundo wa West Ham, kufuatia kipigo hicho lawama kubwa zimeelekezwa kwa beki Marcos Rojo ambae ameonekana kufanya vibaya katika mchezo huo. 

Mchezaji huyo raia wa Argentina anayevaa jezi namba 5 katika klabu hiyo ya Man Utd amebebeshwa lawama hizo na mashabiki wa United akilalamikiwa kushindwa kuzuia krosi zilizokuwa zinapigwa na wachezaji wa West Ham. Rojo amekuwa na wakati mgumu klabuni hapo tangu ajiunge mwaka 2014 akitokea Sporting na ameonekana kuwakera zaidi mashabiki wa United katika mechi yao iliyochezwa jumanne wiki hii.

HIZI HAPA NI BAADHI YA TWEETS ZA MASHABIKI ZIKIELEKEZA LAWAMA KWA ROJO




0 comments:

Post a Comment