Kocha wa klabu ya Tottenham Spurs Mauricio Pochettino amesaini mkataba mpya na klabu hiyo utakaomuweka klabuni hapo hadi mwaka 2021. Pochettino alishatangaza wiki 2 nyuma kuwa alishafanya mazungumzo ya awali na klabu hiyo juu ya kuongeza mkataba na sasa hivi ni rasmi kuwa kocha huyo ataendelea kubaki klabuni hapo.
Kocha huyo mwenye miaka 44 alipewa kibarua cha kuinoa klabu hiyo May 2014 na amekuwa na mafanikio makubwa sana katika klabu hiyo, akiiongoza Tottenham kumaliza katika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza huku wakiwa wamebakisha mchezo mmoja kumaliza ligi nafasi ambayo inawahikikishia kushiriki michuano ya UEFA Champions League msimu ujao.
Kocha msaidizi Jesus Perez, na kocha wa makipa Miguel D’Agostino nao pia wamekubali kuongeza mkataba kuendelea kuitumikia klabu hiyo.
0 comments:
Post a Comment