Shirikisho la Soka Afrika (CAF), limewateua waamuzi wanne kuchezesha mchezo Na. 27 kati ya Ethiopia dhidi ya Ghana kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana 2017 utakaofanyika Uwanja wa Addis Ababa (Gazon Nature), jijini Addis Ababa huko Ethiopia.
Mchezo huo utaochezwa Mei 22, 2016 majira ya saa 10.00 jioni kwa saa za Ethiopia, utaamualiwa na Mfaume Ali Nassoro ayesimama katikati wakati walioteuliwa kuwa waamuzi wa pembeni ni Josephat Deu Bulali (line 1) na Alli Kinduli na mezani atakuwa Martin Eliphas Sanya. Kamishina wa mchezo huo kwa mujibu wa CAF ni Julius Elly Mukolwe kutoka Kenya.
0 comments:
Post a Comment