Friday, May 13, 2016

CAF YATANGAZA MABADILIKO MAKUBWA KLABU BINGWA AFRICA 2017


Maafisa wa shirikisho la kandanda barani afrika (CAF) wamedokeza kuwa kutakuwa na mabadiliko katika ratiba ya michuano ya klabu bingwa barani na ile ya mashirikisho. Rais wa shirikisho hilo Issa Hayatou amethibitisha hayo katika mkutano wa 38 wa maafisa wa (CAF) uliofanyika mjini Mexico kabla ya kongamano la shirikisho la kandanda duniani kufanyika. Katika mabadiliko hayo, timu 16 zitagaeanywa katika makundi manne yaliyo na timu nne badala ya nane. Katika mkutano huo, Hayatou pia alieleza mafanikio ya timu kutoka barani afrika katika mashindano ulimwenguni. Miongoni mwa waliohudhuria mkutano huo ni aliyekuwa mchezaji wa Cameroon Samuel Etoo.

0 comments:

Post a Comment