Friday, May 13, 2016

KLABU 5 TAJIRI ZAIDI DUNIANI 2016


Real Madrid imetajwa kuwa ndio klabu tajiri zaidi duniani kwa mara ya 4 mfululizo, kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Forbes. Wababe hao wa Hispania Walibeba taji la Uefa Super Cup na Klabu Bingwa duniani (Fifa Club World Cup) msimu uliopita na hivi sasa wanakadiriwa kuwa na utajiri wa dola bilioni 3.6 sawa na paundi bilioni 2.5, ikiwa imepanda thamani hiyo kwa asilimia 12% ukilinganisha na mwaka jana.

Madrid inafuatiwa kwa karibu na mahasimu wao wakubwa Barcelona, ambao thamani yao pia imeongezeka kwa asilimia 12% kufikia dola bilioni 3.5 baada ya mafanikio makubwa waliyoyapata mwaka 2015 waliposhinda kombe la Uefa Champions League, La Liga na Copa del Rey.

Manchester United inabaki katika nafasi ya 3 katika orodha hiyo, ikikadiliwa kuwa na utajiri wenye thamani ya dola bilioni 3.3, Wababe wa ligi kuu nchini Ujerumani Bayern Munich katika nafasi ya 4 wakiwa na utajiri wa dola bilioni 2.7 huku klabu inayonolewa na kocha Arsene Wenger ikishika nafasi ya 5 kwa utajiri wa dola bilioni 2.

Klabu zingine za Uingereza katika orodha hiyo ni Manchester City nafasi ya 6 dola bilioni 1.9, ikifuatiwa na Chelsea katika nafasi ya 7 dola bilioni 1.7, Liverpool dola bilioni 1.5 nafasi ya 8, na Tottenham dola bilioni 1 katika nafasi ya 10

0 comments:

Post a Comment