Katika ligi kuu England ni tabia mbaya kwa mchezaji kuonekana
hadharani akivuta sigara, huenda labda ni kutokana na kazi yao wanayofanya ya
kusakata soka ambayo inahitaji uimara wa mwili na akili pia. Na inafikia hatua
makocha wa wachezaji wanaovuta sigara kuwachukulia hatua kali wachezaji hao na
hata kupigwa faini wakati mwingine.
Lakini waswahili husema unapomkataza mtoto kufanya kitu
ambacho wewe mwenyewe unafanya basi unapokuwa unafanya wewe jitahidi ufanyie
sehemu ambapo mtoto wako hatakuona vinginevyo nae lazima atajaribu kufanya ili
aone ni kwanini wewe unamkataza wakati wewe mwenyewe unafanya.
Jurgen Klopp ni kocha wa klabu ya Liverpool inayoshiriki
ligi kuu nchini humo maarufu kama English Premier League, kuvuta sigara imekuwa
ni tabia yake ya siku nyingi na imeonekana kuwa vigumu kwake kuiacha tabia
hiyo, kocha huyo amenaswa akivuta sigara kabla ya kuenda kuongoza kikosi chake
katika mazoezi. Rafiki yake wa karibu anaejulikana kwa jina la Davidi Wegner
alishamzungumzia Klopp kuwa ni mvutaji mkubwa tu wa sigara, alikuwa anafanya
hivyo akiwa na Mainz alifanya pia akiwa na Dortmund na anaendeleza tabia hiyo
hadi hivi sasa alipojiunga na Liverpool.
Jack Wilshere ni mchezaji wa Arsenal ambae alishawahi
kuingia matatani baada ya kunaswa akivuta sigara, kocha wake Arsene Wenger
alilaani sana kitendo hicho.
Wachezaji wengine ambao walishawahi kunaswa wakivuta sigara
ni: Wayne Rooney, Dimitar Berbatov,Fabio Coentrao, Mario Balotelli, Fabien
Barthez na Kocha Carlo Ancelotti nae pia alinaswa akipitia kilevi hicho.
Pata habari za michezo kwa haraka zaidi kupitia soka24.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment