Thursday, June 9, 2016

SAKATA LA UCHAGUZI YANGA, WAGOMBEA WAWEKEWA VIKWAZO

Wote waliochukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi Yanga kupitia TFF wametakiwa kuchua fomu upya katika makao makuu ya klabu ya Yanga.


Wagombea wote waliochukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi Yanga zilizotolewa na TFF wameagizwa kuchukua fomu hizo upya katika klabu ya Yanga. Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi Yanga, Sam Mapande amesema wao kama kamati wamefikia uamuzi huo kwa sababu hawana uhakika kama wote waliochukua fomu hizo TFF ni wanachama halali wa Yanga.

"Hao waliochukua fomu TFF sisi hatuna uhakika kama ni wanachama wa Yanga au la, kwa hiyo wanachotakiwa ni kuomba upya, wapitie taratibu zote za kufanyiwa usaili, wakipitishwa waende kwenye uchaguzi" alisema Sam Mapande.
Hadi hivi sasa tayari wagombea wote waliochukua fomu makao makuu ya klabu ya Yanga wameshaanza kampeni takribani siku 3 zilizopita.

Wanaotakiwa kuchukua upya fomu hizo kwenye makao makuu ya timu hiyo ni;

Titus Osoro na Aaron Nyanda wanawania nafasi ya makamu mwenyekiti, Omari Said, Mchafu Ahmed Chakoma, Paschal Laizer, Edgar Chibula na Mohamed Mattaka hawa wote wanawania ujumbe wa kamati ya utendaji.

0 comments:

Post a Comment