Thursday, June 9, 2016

YALIYOJIRI KESI YA MWINYI KAZIMOTO

Kesi ya mchezaji wa Simba Mwinyi kazimoto kumshambulia na kumdhuru mwandishi wa habari imetolewa maamuzi yalimwacha huru mchezaji huyo .


Kesi hiyo iliyokuwa  inayomkabili mchezaji huyo wa Simba na Timu ya Taifa, Taifa Stars, ya kumshambulia mwanahabari Mwanahiba Richard imetolewa hukumu na  hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Shinyanga Rahim Mushi ambapo na huru Kazimoto baada ya kukutwa hana hatia.

Mwanahiba Richard alidai Mshitakiwa (Mwinyi Kazimoto) alimpiga makofi kwa kile alichodai kumwandia vibaya Kwenye mechi kati ya Simba na Mbeya City iliyochezwa mwaka jana.

Mwanahiba alidai mshitakiwa alimwambia hata kama atampeleka kokote hawatamfanya kitu.

Shahidi wa pili Ndg. Beni Kalama alisema wakati tukio hilo linatokea alienda kuongea na kocha wa Simba ndipo aliposikia kofi linapigwa na alipogeuka kutazama alimwona Mwanahiba akilia.

Kazimoto yeye kwa upande wake alisema alimuuliza mwandishi huyo sababu ya kumuandika vibaya kwenye gazeti lao, wakapishana kauli na ndipo Mwanahiba alipoanza kulia.

Hata hivyo mahakama imeona mchezaji Mwinyi Kazimoto hana hatia hivyo kumwachia huru.

Baada ya hukumu hiyo kusomwa Mwanahiba aliyasema haya;

""Mimi sina maamuzi yoyote, kampuni yangu ndiyo yenye mamlaka katika hili, kwahiyo labda wao ndio wanaweza kusema kama tutakata rufaa au vipi."

0 comments:

Post a Comment