Serikali imetenga kiasi cha Sh. bilioni 3 kwa lengo la kutekeleza miradi mbalimbali ya michezo, sanaa na ubunifu.
Pesa hizo zimetengwa na serikali katika mwaka ujao wa fedha,kwa mujibu wa kauli ya Waziri wa fedha na uchumi Dk. Philip Mpango aliyoitoa bungeni wakati akiwasilisha hotuba ya mapendekezo ya serikali kwa mwaka wa Fedha 2016/17 bungeni mjini Dodoma jana.
"Serikali kupitia fungu 96 imetenga jumla ya shilingi bilioni 3.0 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya sanaa, ubunifu, utamaduni na michezo, ikiwa pamoja na kuratibu na kusimamia uanzishwaji wa mfuko wa maendeleo ya sanaa na ubunifu" alisema Dk. Mpango.
"Kusimamia urasimishaji wa shuguli za sanaa, kusimamia na kudhibiti filamu zitakazoingia sokoni bila kufuata taratibu na kuratibu uendeshaji wa kazi za sanaa nchini" aliongeza Dk. Philip Mpango.
0 comments:
Post a Comment