Wachezaji wa Yanga walipewa mapumziko baada ya fainali ya kombe la shirikisho TFF, Kocha Pluijm ametoa onyo kwa wachezaji wote ambao watachelewa kufika kikosi hapo.
Yanga wameanza mazoezi ya kujiandaa na mchezo wao wa kwanza hatua ya makundi kombe la shirikisho barani Afrika (CAF CC). Kocha mkuu wa klabu hiyo Hans Van Pluijm amesema hatawavumilia wachezaji wote ambao watachelewa kuripoti mapema kambini kujiandaa na michuano hiyo.
"Tunaanzia ugenini na timu ambayo hatuijui sana, hivyo ni lazima kufanya maadalizi ya kutosha ili tukaweze kupambana, hatutaki kwenda kuwa wasindikizaji bali kutafuta taji ambalo ndiyo jambo la msingi kwetu" alisema Pluijm.
Pluijm aliongeza kuwa haoni sababu yoyote ya mchezaji kuchelewa kujiunga na kikosi chake na kwamba atakuwa mkali sana kwa wachezaji ambao watachelewa kuripoti bila kuwa na sababu za msingi.
Yanga inakibarua kizito cha kuhakikisha wanafuzu hatua hii ya makundi na kutinga katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo. Yanga ipo kundi moja na TP Mazembe ya DRC, MO Bejaia ya Algeria na Medeama ya Ghana na itacheza mchezo wake wa kwanza na MO Bejaia wiki moja ijayo huko nchini Algeria.
0 comments:
Post a Comment