Thursday, June 9, 2016

DANIEL AGGER ATANGAZA KUACHANA NA SOKA

Beki wa zamani wa klabu ya Liverpool Daniel Agger ametangaza kustahafu kucheza soka leo alhamisi Juni 9, 2016 akiwa na umri wa miaka 31.


Beki huyo aliyefanikiwa kuichezea timu yake ya taifa ya Denmark mechi 71 alishare taarifa hiyo pia katika akaunti yake ya Twitter na kuandika maneno haya;

"Asanteni wote kwa sapoti yenu. Ni uzoefu mkubwa, Inahuzunisha lakini ni maamuzi sahihi kupumzika. Ninajivunia kazi yangu."


Agger ameitumikia Liverpool kwa miaka 8 tangu ajiunge mwaka 2006. Akiwa Anfield alikuwa moja kati ya mabeki bora katika ligi kuu nchini Uingereza na kufanikiwa kushinda kombe la ligi akiwa na Majogoo hao wa London mwaka 2012.

0 comments:

Post a Comment