Thursday, June 9, 2016

MESSI HANA HARAKA YA KUONGEZA MKATABA BARCELONA

Supastaa wa soka duniani Lionel Messi hajaanza mazungumzo ya kuongeza mkataba wake uliosalia miaka 2 katika klabu yake ya Barcelona.


Barcelona hawajaanza mazungumzo ya kuongeza mkataba wa Messi unaomalizika miaka 2 ijayo.
Messi hajapokea maombi yoyote ya kuongeza mkataba kutoka kwa uongozi wa Barcelona huku yeye mwenyewe akionekana kutokuwa na haraka na jambo hilo.

Kumekuwa na ripoti zinazosema kuwa Barcelona wamepanga kumpa mkataba mrefu zaidi Messi utakaomfanya kukaa klabuni hapo hadi anafikisha umri wa miaka 35 licha ya Mourinho kutuma Ofa mara mbili akimuhitaji nyota huyo.

Kwa sasa Messi yupo Marekani katika michuano ya Copa America akiiwakilisha nchi yake ya Argentina katika michuano hiyo.

Siku chache zilizopita kumekuwa na uvumi kuwa kocha mpya wa United, Jose Mourinho ametuma Ofa mbili katika klabu ya Barcelona akihitaji kumsajili Lionel Messi.

0 comments:

Post a Comment