Shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania TFF limetangaza tarehe ya kuanza kwa zoezi la usajili kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu Vodacom Tanzania kuwa ni Juni 15 hadi Agosti 6, 2016.
Kwa mujibu wa kalenda ya shirikisho hilo, usajili utaanza rasmi Juni 15 na kufungwa Julai 30, 2016.
Kuanzia Juni 15 hadi Julai 30 timu zote zinazoshiriki ligi kuu Vodacom zitatumia kutangaza wachezaji wanaowaacha na kusajili wapya.
Pingamizi itakuwa Agosti 7 hadi 14, 2016, uthibitishwaji wa usajili hatua ya kwanza ni kati ya Agosti 15 na Agosti 19.
Usajili hatua ya pili ni Agosti 17 hadi Septemba 7, 2016 na kipindi cha pingamizi hatua ya pili ni kuanzia Septemba 8 hadi Septemba 14.
Septemba 15 hadi Septemba 17 ni kipindi cha kuthibitisha usajili hatua ya pili.
Timu zimetakiwa kuanza maadalizi kuanzia Juni 15 hadi Julai 15, 2016 na kuanzia Julai 16, 2016 hadi Agosti 14 ni kipindi cha mechi za kirafiki za ndani na nje.
Ratiba ya Ligi kuu Vodacom msimu ujao wa 2016/17 inatarajiwa kutoka kati ya Julai 16 hadi Agosti 14, 2016.
0 comments:
Post a Comment