Thursday, June 9, 2016

MJUE ERIC BAILLY NYOTA ALIYETUA MAN U

Klabu ya Manchester United imefanikiwa kumsajili Eric Bailly kutoka katika klabu ya Villarreal, Soka24 inakujuza kiundani zaidi kuhusu mchezaji huyu.


JINA KAMILI; Eric Bertrand Bailly
KUZALIWA; April 12, 1994
MAHALA ALIPOZALIWA; Bingerville, Ivory Coast
UMRI; Miaka 22
URAIA; Ivory Coast
UREFU; 1.87 m ( futi 6 na inch 1.5)

UTANGULIZI
Eric Bailly amekuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Jose Mourinho katika klabu ya Manchester United akitokea Villarreal kwa kitita cha paundi milioni 30.

Beki huyo wa kati amesaini kandarasi ya miaka minne (4) kuitumikia klabu hiyo.

Bailly ni mchezaji ambaye anajua vizuri nini anachokifanya anapokuwa uwanjanai. Miaka 5 iliyopita, Emilio Montagut alikiona kipaji chake akiwa katika mashindano ya vijana huko Burkina Faso na bila kuchelewa alifanya taratibu za kumhamishia katika kikosi cha Espanyol B, napo hakuchelewa akachukuliwa kikosi cha wakubwa kabla hajasajiliwa na  Villarreal kwa uhamisho wa paundi milioni 4.4 . akiwa La liga Bailly alionyesha kiwango kikubwa katika mechi 35 alizofanikiwa kucheza na tayari kocha Mourinho akaona kipaji chake na hivi sasa ameshatua Man U kwa kitita cha paundi milioni 30.

Akiwa Villarreal mwaka 2005, Bailly aliitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Ivory Coast na alikuwa na mchango mkubwa katika timu yake na alikuwa ni miongoni mwa wachezaji waliobeba kombe la mataifa ya Afrika yaliyofanyika nchini Gambia, alicheza mechi zote sita katika mashindano hayo na kufanikiwa kufunga goli moja katika mikwaju ya penati, wakati Ivory Coast ilipotwaa ubingwa wa AFCON dhidi ya Ghana.

Villarreal walimsajili Bailly kama mbadala wa Gabriel Paulista na aliziba vizuri pengo hilo.
Aidha Bailly ni miongoni mwa wachezaji ambao waliifanya Villarreal kucheza mechi 17 bila kuruhusu goli lolote katika lango lao katika La Liga msimu huu na aliisaidia timu yake pia kufika hatua ya nusu fainali ya Europa League ambapo walikuja kutolewa na Liverpool.

Bailly ni Mrefu, Imara, na mwepesi katika kufanya maamuzi uwanjani. Kwa rekodi zake katika mechi alizocheza ni wazi kuwa atakuwa na mchango mkubwa katika klabu ya Manchester United.

HISTORIA YAKE FUPI KATIKA SOKA

Bailly alijiunga na kikosi cha vijana cha RCD Espanyol Disemba 2011 akiwa na umri wa miaka 17, lakini Octoba 5, 2014 ndipo Bailly alicheza mechi yake ya kwanza ya ligi kuu nchini Hispania La Liga, akitokea benchi, mechi ambayo Espanyol ilishinda 2 - 0 dhidi ya Real Sociedad.
Januari 29, 2015, Bailly alisaini mkataba wa miaka 5 na nusu katika klabu ya Villarreal kwa uhamisho wa Euro milioni 5.7 na alicheza mechi yake ya kwanza Februari 22, na timu yake kufanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1 - 0 dhidi ya SD Eibar.

March 19, 2015, Bailly alicheza mchezo wake wa kwanza wa Europa League akianza katika kikosi cha kwanza katika mechi na Sevilla na baadae alitolewa nje katika mchezo huo ambao Villarreal ilipoteza 2 - 1 dhidi ya Sevilla.

Alicheza mechi 7 katika michuano hiyo ya Europa msimu huo, na alifanikiwa kufunga goli 1 katika ushindi wa 4 - 0 dhidi ya FC Dinamo Minsk.

Juni 8, 2016, Bailly amesaini mkataba wa miaka 4 katika klabu ya Man U na anaweza pia kuongeza miaka 2 zaidi kama atapenda.

NAFASI YAKE KATIKA KIKOSI CHA MANCHESTER UNITED

Kufuatia kuonyeshwa mlango wa kutokea kwa Daley Blind ni wazi kuwa Bailly atachukua nafasi hiyo akishirikiana kwa ukaribu na Chris Smalling na Luke Shaw beki ya kushoto huku Matteo Darmian akisimama kama full Back.

Nafasi ya beki wa kati ilionekana kuwa na changamoto kubwa katika kipindi cha Van Gaal na sasa imani kubwa ya wapenzi wa Manchester United ni kuona Bailly akiimudu vizuri nafasi hiyo.


Related Posts:

  • Rasmi: Torino Yamnasa Joe Hart Mlinda Mlango namba moja wa Uingereza Joe Hart amekamilisha uhamisho wa kujiunga na Klabu ya Torino inayoshiriki ligi kuu nchini Italia kwa mkopo akitokea Manchester City. Hart alijikuta akiwa chaguo la pili la kocha Pep … Read More
  • Arsenal Yakamilisha Usajili Wa Shkodran Mustafi Klabu ya Arsenal imetangaza rasmi kumsajili beki wa kati wa Valencia Shkodran Mustafi kwa ada ya uhamisho ambayo haijawekwa wazi. Licha ya thamani ya uhamisho wa mchezaji huyo kutowekwa wazi lakini habari za chini chini z… Read More
  • Rasmi:Samir Nasri Atua Sevilla Manchester City imetangaza kuwa Samir Nasri amejiunga na klabu ya Sevilla kwa Mkopo. Endelea Kuungana Na Soka24 kwa habari za papo kwa papo za Soka kote Ulimwenguni............. ================== Stori Kubwa Zinazotikisa… Read More
  • YAYA TOURE ATUPWA NJE YA KIKOSI CHA MAN CITY Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amemwacha nje kiungo wa kati wa timu hiyo yaya Toure katika kikosi chake cha kombe la vilabu bingwa Ulaya mwaka 2016-17. City haikuweza kuweka zaidi ya wachezaji 17 wa kigeni katika kik… Read More
  • USIPITWE NA HAYA MAMBO MUHIMU USAJILI LIGI KUU UINGEREZA 2016-17 Klabu za Ligi ya Premia zilitumia zaidi ya £155m siku ya mwisho ya kuhama kwa wachezaji kipindi cha majira ya joto na kufikisha jumla ya pesa zilizotumiwa hadi rekodi mpya ya £1.165bn. Klabu zilikuwa tayari zimetumia j… Read More

0 comments:

Post a Comment