Christiano Ronaldo amefunga magoli mawili katika mchezo huo wa kujiandaa na michuano ya Euro 2016, magoli aliyofunga katika dakika ya 36' na 45.
Magoli mengine yalifungwa na Ricardo Quaresma naye pia akifunga mawili dakika ya 39' na 77', Danilo dakika ya 55', Eder dakika ya 80' na goli la kujifunga la Metis katika dakika ya 61'.
Mchezo huo ulikuwa ni wa kwanza kwa Ronaldo tangu acheze mechi ya fainali ya Uefa Champions League, mwezi uliopita.
Ronaldo kwa sasa amefikisha jumla ya magoli 58 katika timu yake ya taifa ya Ureno.
Ureno watacheza mchezo wao wa kwanza katika michuano ya Euro huko Ufaransa katika kundi F dhidi ya Iceland siku ya Jumanne.
0 comments:
Post a Comment