Wakati akihusihusishwa na tetesi za kuondoka klabuni hapo Mephis Depay amefuta
picha zake zote instagram, kitu ambacho ni kama ishara tosha kuwa Mdachi huyo
yupo mbioni kutimka klabuni hapo akiwa ameitumikia klabu hiyo kwa muda wa mwaka
mmoja tu.
Picha zake zote alizopiga akiwa Man Utd amezifuta, huku pia
akiwa ameacha kuwa-follow wachezaji wenzie wote( yani amewa-unfollow) wa klabu
hiyo ya Manchester United.
Depay bado anaendelea kui-follow klabu ya Man United katika
account yake ya Instagram na kwenye akaunti yake ya twitter bado ziko picha
ambazo anaonekana akiwa amevaa jezi ya Man United.
Mephis Depay alisaini katika klabu ya Manchester United
Msimu uliopita kwa ada ya paundi milioni 31. Tangu ajiunge na Mashetani hao
winga huyo ameshindwa kuonyesha kiwango kizuri akifanikiwa kufunga magoli 2 tu
katika michezo 15 aliyocheza.
Wiki chache zilizopita tetesi zilikuwa zinamhusisha Depay na
kuondoka klabuni hapo baada ya
kuitumikia klabu kwa msimu mmoja tu.
Pata habari za michezo kwa haraka zaidi kupitia soka24.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment