Saturday, April 30, 2016

YANGA YAZIDI KUCHANJA MBUGA KAZI IMEBAKI KWA AZAM NA SIMBA


LIGI Kuu Tanzania Bara imeendelea tena hivi leo katika viwanja 4, huko Jijini Mwanza wenyeji Toto Africans Wakiikaribisha Yanga. Mchezo huo ulioshuhudiwa na maelfu ya watazamaji ulikuwa na wa kuvutia ukizingatia kwamba timu hizo mbili licha ya kuhusishwa na undugu leo ziliingia uwanjani kila moja ikihitaji ushindi katika mchezo huo.
Toto ndo walikuwa wa kwanza kupata goli kipindi cha kwanza cha mchezo dakika ya 39 goli lililofungwa na William Kimanzi kwa kichwa akiunganisha vizuri mpira wa kona. Hadi timu zinakwenda mapumziko Toto walikuwa mbele kwa goli 1. Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ya kawaida Yanga wakipeleka mashambulizi mengi langoni kwa Toto na hatimaye Hamisi Tambwe aliisawazishia timu yake goli la kwanza kabla ya Juma Abdul kuifungia Yanga goli la pili na la ushindi. Yanga inafikisha pointi 65 katika nafasi ya kwanza, huku wakisubiri matokeo ya mahasimu wao Azam na Simba wanaocheza kesho Jumapili.

Michezo mingine ni:
African Sports 1 - 0 Coastal Union









Pata habari za michezo kwa haraka zaidi kupitia soka24.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment