Monday, May 2, 2016

RUFAA HIZI 8 KUTOLEWA MAAMUZI NA KAMATI YA RUFAA YA NIDHAMU TFF KESHO


Kamati ya Rufaa ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kesho Jumanne Mei 3, 2016 saa 5:00 asubuhi itatangaza uamuzi wa rufaa nane zilizowasilishwa na kujadiliwa za viongozi, mchezaji na timu tatu zilizoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara 2015/2016.

Kamati hiyo itatangaza uamuzi huo mbele ya waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Mikutano wa ofisi za TFF, zilizoko kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.

Jumla ya rufaa nane zinazohusu timu, kocha, viongozi na mchezaji mmoja zilijadilikuwa na kamati hiyo kwa Jumapili Mei mosi, 2016 kwenye ofisi za TFF jijini.

Rufaa zilizojadiliwa kwenye kikao hicho ni za:

1.   Timu ya Geita Gold

2.   Choki Abeid ambaye ni Kocha Msaidizi wa timu ya soka ya Geita Gold FC

3.   Denis Richard Dioniz - Kipa wa Geita Gold

4.   Fatel Rhemtullah – Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Tabora

5.   Saleh Mang’ola – Mwamuzi wa Soka wa Mkoa wa Dodoma

6.   Timu ya Soka ya Polisi Tabora

7.   JKT Oljoro Fc ya Arusha

8.   Yusufu Kitumbo – Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Tabora

Wadau hao wa soka walikata rufaa dhidi ya uamuzi wa Kamati ya Nidhamu baada ya kamati hiyo kuwatia hatiani na kuwaadhibu kwa makosa ya kupanga matokeo ya michuano ya Ligi Daraja la Kwanza. Wakata rufaa wote walihudhuria kikao cha rufaa zao.    

chanzo: TFF Official site
Pata habari za michezo kwa haraka zaidi kupitia soka24.blogspot.com

Related Posts:

  • SIMBA YAPEWA ONYO MBEYA Timu ya soka ya Simba inatarajiwa kushuka katika dimba la Sokoine Jijini Mbeya siku ya jumatano kuvaana na timu ya wananchi kutoka jijini humo Mbeya City. Kuelekea Mchezo huo, Klabu ya Mbeya City imetoa onyo kwa Wekundu h… Read More
  • MCHEZO WA STARS NA ETHIOPIA WAYEYUKA Lile pambano lililokuwa linasubiriwa kwa hamu na wapenzi wengi wa soka nchini limeota mbawa baada ya shirikisho la soka la Ethiopia kuiandikia TFF kuwa mchezo huo hautakuwepo kutokana na sababu za kiusalama nchini Ethiopia… Read More
  • MO,MANJI KIKAANGONI OCTOBA 20,2016 CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), kimeandaa kongamano maalumu Oktoba 20 mwaka huu, kuzungumzia mifumo ya kiuendeshaji ambayo klabu kongwe nchini za Simba na Yanga zipo mbioni kuingia. Simba na Yan… Read More
  • TAARIFA YA YANGA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU KUKODISHA TIMU TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI MUHTASARI WA MKATABA.  1. Bodi ya Wadhamini wa Young Africans Sports Club, (ambayo hapa inajulikana kama Mmiliki”) imeingia tarehe 3 September, 2016 Mkataba wa kukodishwa na kampuni iju… Read More
  • VIONGOZI TOTO AFRICANS WATUMBULIWA Uongozi wa klabu ya Toto Africans ya jijini Mwanza umewasimamisha baadhi ya viongozi wake kutokana na kile kilichotajwa kuwa ni utovu wa nidhamu. Godwin Aiko, Mwenyekiti wa klabu hiyo amesema sababu kubwa ya kuwasimamisha… Read More

0 comments:

Post a Comment