Sunday, June 5, 2016

BEKI KISIKI WA GORMAHIA AOMBA KUJIUNGA NA SIMBA SC AJE KUONYESHA KAZI

Beki wa Gormahia ya nchini Kenya Karim Nzigiyimana ameweka wazi kuwa yupo tayari kujiunga na Simba SC, kwani kwa muda mrefu amekuwa akitamani kucheza Ligi kuu Nchini Tanzania.




Karim Nzigiyimana amesema yupo tayari kujiunga na vijana wa Msimbazi ikiwa pia ni kama kuziba pengo la Hassan Ramadhani "Kessy" aliyetimkia katika klabu ya Yanga.
Nzigiyimana amesema anavutiwa sana na Ligi Kuu Tanzania na kucheza katika Ligi hiyo atakuwa anatimiza ndoto yake ya muda mrefu.

"Nimepigiwa simu na rafiki yangu wa karibu na ameniambia Simba naweza kupata nafasi, nitafurahi kama nikweli kwasababu siku nyingi nimekuwa nikiwaza kucheza ligi ya Vodacom kutokana na ushindani uliopo nitafurahi kama nitakuja hapo" alisema Nzigiyimana alipoongea na Goal.

0 comments:

Post a Comment