Sunday, May 1, 2016

DI MARIA NA IBRAHIMOVIC WANG'AA WAKATI PSG IKIIADHIBU RENNES



VIGOGO wa ligi ya Ufaransa Ligue 1, wameendeleza ubabe wao tena jana kwa kuishushia kichapo kikali cha magoli 4 - 0 timu ya Rennes, mchezo uliopigwa katika dimba linalomilikiwa na Paris Saint-Germain, Parc des Princes.

Di Maria na Ibrahimovic walionyesha kiwango bora katika mchezo huo, huku Ibrahimovic akifanikiwa kufunga magoli mawili dakika ya 54 na 78.
Magoli mengine ya PSG yalifungwa na Maxwell 50' na la 4 lilifungwa na Cavani dakika za nyongeza za mchezo.

Matokeo hayo yameifanya PSG kufikisha pointi 89 katika michezo 35, wakishika nafasi ya kwanza huku wakifuatiwa kwa mbali na Olympique Lyonnais waliojikusanyia pointi 69 katika nafasi ya pili huku wakiwa wameshacheza michezo 36.




Pata habari za michezo kwa haraka zaidi kupitia soka24.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment