Monday, June 6, 2016

ZLATAN IBRAHIMOVIC ATAJA TAREHE ATAKAYOTANGAZA TIMU ANAYOJIUNGA NAYO

Straika Mswedish Zlatan Ibrahimovic aliyekataa kuongeza mkataba na klabu yake ya PSG amesema ifikapo Juni 7, 2016 ndipo ataweka wazi klabu ambayo anajiunga nayo.


Zlatan Ibrahimovic anatarajia kutangaza wapi anatarajia kwenda kucheza soka baada ya kutoka PSG Jumanne hii Juni 7. Zlatan kwa muda mrefu amekuwa akihusishwa kujiunga na klabu ya Manchester United tangu atangaze kuondoka PSG.

"Kutakuwa na tangazo kubwa sana Juni 7. Litakuwa ni bomu kubwa kwa msimu huu wa usajili" alisema Zlatan alipozungumza na Televisheni ya nchini Sweden.

Zlatan Ibrahimovic kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kuamua kutokuongeza mkataba na klabu yake ya PSG, na tangu atangaze uamuzi huo, amekuwa akihusishwa na kutua Old Trafford kufanya kazi tena na Bosi wake wa zamani Jose Mourinho.

0 comments:

Post a Comment