Sunday, July 10, 2016

UMRI HALISI WA RENATO SANCHES WAJULIKANA

Hivi karibuni kumekuwa na shaka juu ya umri halisi wa mchezaji wa Ureno Renato Sanches kwamba mchezaji huyo ana miaka kati ya 23 au 24 na sio 18 kama ambavyo mwenyewe anasema.

Ushahidi wa vipimo kutoka hospitalini unaonesha kuwa mchezaji huyo ana umri wa miaka 18 kama ambavyo mwenyewe alikuwa anasema na si vinginevyo.

Kocha mkongwe wa Ufaransa alizua mijadala mizito katika vyombo mbalimbali vya habari pamoja na mitandao ya kijamii pale aliposema mchezaji huyo wa klabu ya Bayern Munich raia wa Ureno amedanganya umri.
Cheti Cha Kuzaliwa Cha Renato Sanches, Angalia Sehemu iliyozungushiwa kwa rangi ya Njano

Baada ya Vipimo hivyo Sanches alisema "Nimekulia Ureno, Nimekaa miaka 10 Benifica, nawezaje kuwa na miaka 25?"

Sanches alitiliwa shaka juu ya umri wake kutokana na uwezo wake mkubwa uwanjani lakini ukweli ni kwamba nyota huyo ana miaka 18 tu na si 24 au 25 kama ambavyo kocha huyo wa Ufaransa alisema.
Bonyeza Hapa Ku-Like Ukurasa Wa Soka24 Facebook

0 comments:

Post a Comment