Saturday, July 9, 2016

NYOTA WATATU YANGA KUKOSA MCHEZO DHIDI YA MEDEAMA

Klabu ya Yanga inaendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo wa kombe la shirikisho Barani Afrika hatua ya makundi dhidi ya Medeama kutoka nchini Ghana lakini huenda wachezaji wake watatu wakaukosa mchezo huo kutokana na sababu mbalimbali.

Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh amewataja wachezaji hao kuwa ni Mwinyi Haji na Geofrey Mwashiuya wanaosumbuliwa na maumivu ya goti wakati Deus Kaseke yeye anauguza majeraha aliyoyapata baada ya kupata ajali ya pikipiki.

"Tuna majeruhi watatu hadi sasa wanaendelea kupatiwa matibabu,bado hawajaanza mazoezi yoyote, lakini wachezaji wengine wote wanaendelea na mazoezi vizuri" alisema.

Aidha Mchezaji Juma Mahadhi ambaye aliumia katika mchezo dhidi ya TP Mazembe amepona na tayari anaendelea na mazoezi na wachezaji wenzake kujiandaa na mchezo huo dhidi ya Medeam FC.
Chirwa ambaye alikwenda nchini kwao kwa ajili ya mchezo dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia Congo amesharejea na yupo tayari kwa ajili ya mchezo huo.

Yanga imekwishacheza mechi mbili katika hatua hiyo ya makundi na wamepoteza katika michezo yote miwili na kushika nafasi ya mwisho katika msimamo wa kundi A, huku TP Mazembe akiwa kinara wa kundi hilo kwa kujikusanyia alama 6 katika michezo yote miwili aliyocheza.
Bonyeza Hapa Ku-Like Ukurasa Wa Soka24 Facebook



1 comments:

  1. Kazi nzuri endeleeni kuwajuza wananchi yanayoendelea kujiri.

    ReplyDelete