Saturday, July 9, 2016

MNIGERIA AHMED MUSA ATUA LEICESTER CITY

Klabu ya Leicester City imemsajili mshambuliaji wa Nigeria Ahmed Musa kutoka CSKA Moscow kwa mkataba wa miaka 4 utakaogharimu pauni milioni 16.

Southampton,Everton na West Ham walikuwa wakitafuta saini ya mchezaji huyo.
Musa ni mchezaji wa nne kusajiliwa na Leicester baada ya kipa Ron-Robert Zieler ,beki Luis Hernandez na kiungo wa kati Nampalys Mendy.

Mchezaji huyo alijiunga na CSKA mwaka 2012 na kufunga mabao 54 kati ya mechi 168 alizocheza,na amefunga mabao 11 katika mechi 58 alizochezea Nigeria tangu aanze kucheza mwaka 2010.
Bonyeza Hapa Ku-Like Ukurasa Wa Soka24 Facebook

0 comments:

Post a Comment