Saturday, July 9, 2016

SHIZA KICHUYA ATUA MSIMBAZI

Klabu ya Mtibwa Sugar imethibitisha kukamilisha uhamisho wa mchezaji wao Shiza Kichuya kujiunga na klabu ya Simba.

Kwa muda mrefu kichuya alikuwa akihusishwa na kujiunga na wekundu hao wa Msimbazi lakini taarifa za hivi punde ni kwamba tayari Mtibwa wameshamalizana na Simba kuhusu uhamisho wa mchezaji huyo.

"Tayari tumekamilisha dili la kumuuza Kichuya, kwa hiyo ameshajiunga na wenzake wa Simba, ni mchezaji mzuri tunasikitika lakini hatuna jinsi, tutaangalia wengine wa kuziba pengo lake" alisema Kifaru.

Kichuya anakuwa mchezaji wa tatu kujiunga na Simba akitokea Mtibwa Sugar wengine wakiwa ni Mohamed Ibrahim na Muzamil Yasin.
Bonyeza Hapa Ku-Like Ukurasa Wa Soka24 Facebook

0 comments:

Post a Comment