Saturday, July 9, 2016

NYOTA WATATU YANGA KUKOSA MCHEZO DHIDI YA MEDEAMA

Klabu ya Yanga inaendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo wa kombe la shirikisho Barani Afrika hatua ya makundi dhidi ya Medeama kutoka nchini Ghana lakini huenda wachezaji wake watatu wakaukosa mchezo huo kutokana na sababu mbalimbali.

Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh amewataja wachezaji hao kuwa ni Mwinyi Haji na Geofrey Mwashiuya wanaosumbuliwa na maumivu ya goti wakati Deus Kaseke yeye anauguza majeraha aliyoyapata baada ya kupata ajali ya pikipiki.

"Tuna majeruhi watatu hadi sasa wanaendelea kupatiwa matibabu,bado hawajaanza mazoezi yoyote, lakini wachezaji wengine wote wanaendelea na mazoezi vizuri" alisema.

Aidha Mchezaji Juma Mahadhi ambaye aliumia katika mchezo dhidi ya TP Mazembe amepona na tayari anaendelea na mazoezi na wachezaji wenzake kujiandaa na mchezo huo dhidi ya Medeam FC.
Chirwa ambaye alikwenda nchini kwao kwa ajili ya mchezo dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia Congo amesharejea na yupo tayari kwa ajili ya mchezo huo.

Yanga imekwishacheza mechi mbili katika hatua hiyo ya makundi na wamepoteza katika michezo yote miwili na kushika nafasi ya mwisho katika msimamo wa kundi A, huku TP Mazembe akiwa kinara wa kundi hilo kwa kujikusanyia alama 6 katika michezo yote miwili aliyocheza.
Bonyeza Hapa Ku-Like Ukurasa Wa Soka24 Facebook



Related Posts:

  • MSIMAMO MAKUNDI YOTE KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA (CAF CC) MSIMAMO MAKUNDI YOTE KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA (CAF CC) Ungana Na Soka24 Facebook, Bonyeza  HAPA  Kwa Habari Za Haraka Za Soka Kote Ulimwenguni. … Read More
  • MEDEAMA KUTUA DAR KESHO Wapinzani wa Yanga katika mchezo ujao wa Kombe la Shirikisho Afrika, Medeama ya Ghana wanatarajiwa kutua nchini kesho tayari kwa mchezo wa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Yanga katika msimamo wa Kund… Read More
  • MEDEAMA YAICHIMBA MKWARA YANGA Klabu ya Medeama SC imetoa onyo kwa Yanga kuelekea mchezo wao wa marudiano utakaofanyika siku ya Jumatano huko nchini Ghana. Mkwara huo umekuja baada ya Medeama kushinda katika mchezo wake dhidi ya Liberty Professionals w… Read More
  • HIKI NDO KIKOSI CHA YANGA DHIDI YA MEDEAMA SC LEO KOMBE LA SHIRIKISHO BARANI AFRIKA (CAF CC) 2016HATUA YA MAKUNDIMCHEZO WA KUNDI A YANGA SC VS MEDEMA SC KIKOSI CHA YANGA LEO  1. Deogratius Bonaventura Munishi  2. Juma Abdul Mnyamani. 3. Oscar Fanuel Joshua. … Read More
  • KAULI ZA WACHEZAJI YANGA KUELEKEA MECHI DHIDI YA MEDEAMA Mabingwa wa Ligi kuu Vodacom na Wawakilishi pekee Afrika Mashariki katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika klabu ya Yanga inatarajiwa kushuka dimbani kesho kumenyana na Medeama SC kutoka nchini Ghana mchezo wa tatu hat… Read More

1 comments:

  1. Kazi nzuri endeleeni kuwajuza wananchi yanayoendelea kujiri.

    ReplyDelete