Baba mzazi wa Sergio Aguero amesema kijana wake ataachana na timu ya taifa ya Argentina endapo Messi hatakubali kurudi tena kikosini.
Aguero amekuwa rafiki wa mkubwa na wakaribu sana kwa Messi tangu wakiwa na kikosi cha vijana cha timu ya taifa ya Argentina chini ya umri wa miaka 20. Na hata baada ya kipigo walichopokea kwenye fainali ya Copa America kutoka kwa Chile, Messi alienda nyumbani kwa Aguero mjini Rosario.
"Kama Leo hatarudi kwenye kikosi cha timu ya Taifa, Sergio nae atastaafu timu ya taifa" alisema Leonel Aguero, baba yake Aguero.
"Ataondoka na kuwaachia vijana chipukizi kama ambavyo wanahabari wamekuwa wakiandika na kusema kuwa wakati wao Messi na Aguero umekwisha katika timu ya taifa"
Aidha baba huyo wa nyota wa Manchester City alisema kuwa kazi ya Gerardo Martino katika kikosi cha timu ya taifa ya Argentina haikuwa mzuri.
"Unatakiwa kucheza na kushinda katika mechi za fainali, Timu ilitoa faida kwa Chile, tulikuwa tunacheza tukiwa na majeruhi watatu uwanjani na tuliwazawadia dakika 60" aliongeza Leonel.
Hakuishia hapo tu, Mzee huyo aliendelea kusema kuwa katika mechi chache za mwanzo ilionekana kana kwamba Argentina itashinda katika kila mchezo lakini baada ya matokeo mabaya ya fainali, stori ilibaki kuwa ileile ya siku zote.
"Wanamlaumu kila mtu, wanamlaumu Messi ambaye anajitolea kila kitu kwa ajili ya timu"

0 comments:
Post a Comment