Saturday, June 4, 2016

USAIN BOLT KUPOKONYWA MEDALI YAKE YA DHAHABU

Bingwa wa dunia katika mbio za mita 100 na 200 Mjamaika Usain Bolt huenda akapokonywa moja ya medali zake za dhahaabu alizoshinda katika michizo ya Olimpiki iliyofanyika mjini Beijing 2008.




Hali hiyo inakuja kufuatia chombo cha Reuters kuripoti kwamba washiriki katika kikosi cha Jamaica kilichokimbia mbio za kupokezana vijiti za 4 mara 100, Mmoja wa washiriki hao, Nesta Carter alipatikana na dawa za kusisimua misuli.
Nesta Carter



Carter alipimwa na kukutwa na hatia hiyo na kamati ya Olimpiki ya kimataifa itamfanyia tena vipimo na ikigundulika kwa mara pili basi Carter atawekewa vikwazo.

Carter na wakala wake hawajatoa tamko lolote kuhusiana na tuhuma hizo.

0 comments:

Post a Comment