Mlinzi wa kati wa klabu ya Villarreal ya nchini Hispania Eric Bailly huenda akawa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Mourinho katika klabu ya Man United.
Ripoti kutoka ndani ya klabu ya Man U zinasema wameshafikia makubaliano na Bailly 22, na kwamba kinachosubiriwa hivi sasa ni vipimo tu, endapo matokeo ya vipimo hivyo yatakuja vizuri basi Bailly atakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na kocha Mourinho mara baada ya kujiunga na Mashetani wekundu.
Uhamisho huo wa Bailly kutoka Villarreal utawagharimu United kitita cha paundi milioni 30.
Zlatan Ibrahimovic ndiye alitarajiwa kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na United lakini hadi hivi sasa mambo yamekuwa kimya.
0 comments:
Post a Comment