Friday, May 20, 2016

MOURINHO NA VAN GAAL KUFANYA KAZI PAMOJA UNITED

Man U wameripoti kwamba wameamua kufanya mabadiliko ya Uongozi wa juu lakini Van Gaal atabaki United.



Louis Van Gaal atapewa majukumu ya juu ya utawala katika klabu hiyo ili kumpisha Mourinho kuchukua nafasi hapo United. Mourinho amehusishwa kwa muda mrefu sasa kuhamia Old Trafford baada ya Msimu mbaya wa timu chini ya Van Gaal. Na inaonekana kwamba kufeli kwa Van Gaal kuifikisha timu katika nafasi ya Kushiriki UEFA Champions Msimu Ujao Kumefanya Mfumo wa uongozi United kutaka kufanya mabadiliko ya kiutawala.

Lakini ripoti ya The Sun inasema Van Gaal anafikiriwa sana na Mkurugenzi wa United Ed Woodward kupewa nafasi ya Ukurugenzi katika majukumu ya soka klabuni hapo. Van Gaal amebakisha mwaka mmoja katika mkataba wake, hivyo kupandishwa kwake kutoka ukocha hadi Ukurugenzi kutampa nafasi ya kumalizia mkataba wake huku akimpa Mourinho nafasi ya kuwa kocha.

United Itakosa michuano ya UEFA Champions kwa mara ya pili katika misimu mitatu.

Related Posts:

  • UZI MPYA WA MANCHESTER UNITED MSIMU UJAO Klabu ya Manchester United imetoa jezi zake mpya zitakazotumiwa katika msimu ujao wa ligi kuu Uingereza. Jezi mpya za Man U msimu ujao Bei: Shirt ni Pauni 60 (Tsh.172862) kwa wakubwa na ukihitaji ya mikono mirefu inakuwa … Read More
  • MNIGERIA AHMED MUSA ATUA LEICESTER CITY Klabu ya Leicester City imemsajili mshambuliaji wa Nigeria Ahmed Musa kutoka CSKA Moscow kwa mkataba wa miaka 4 utakaogharimu pauni milioni 16. Southampton,Everton na West Ham walikuwa wakitafuta saini ya mchezaji huyo. M… Read More
  • RASMI: MANCHESTER CITY YAMNASA MORENO Klabu ya Manchester City iliyo chini ya kocha Mpya Pep Guardiola imekamilisha uhamisho wa kinda Mkolombia Marlos Moreno. Moreno 19, ametua katika dimba la Etihad akitokea Atletico Nocional na amesaini mkataba wa miaka mit… Read More
  • SUNDERLAND YAMRUDISHA DAVID MOYES UINGEREZA Klabu ya Sunderland imemteua kocha wa zamani wa Manchester United David Moyes kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo baada ya Sam Allardyce kukabidhiwa kikosi cha timu ya taifa ya England. Moyes anachukua mikoba ya Sam Allardyce k… Read More
  • VIDEO: INTERVIEW YA KWANZA YA DAVID MOYES SUNDERLAND David Moyes ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa klabu ya Sunderland akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Sam Allardyce aliyekabidhiwa timu ya taifa ya Uingereza. Hii hapa chini Interview Yake ya kwanza mara tu baada ya kutang… Read More

0 comments:

Post a Comment