Sunday, June 26, 2016

MOURINHO AKERWA NA MAAMUZI YA ED WOODWARD

Kocha mpya wa Man U Jose Mourinho amekerwa na kitendo cha bosi wake Ed Woodward kushindwa kukamilisha dili la Renato Sanches.

United tayari imeshakamilisha usajili wa mlinzi kutoka Villarreal, Eric Bailly kwa uhamisho wa paundi milioni 30 lakini amekerwa na kitendo cha kumkosa Renato Sanches.

Mourinho amepewa paundi milioni 200 za kufanyia usajili msimu huu, kwa muda mrefu Mourinho alikuwa anahitaji huduma ya Sanches lakini mchezaji huyo ameishia kujiunga na wababe wa ligi ya Ujerumani, Bayern Munich akitokea katika klabu ya Benifa.

Hata hivyo Mourinho amepanga kuongeza wachezaji wengine wanne, Zlatan Ibrahimovic akiwa mmoja wa wanaohusishwa na kujiunga na United.

Bonyeza Hapa Ku-Like Ukurasa Wa Soka24 Facebook

0 comments:

Post a Comment