Sunday, June 26, 2016

HATIMAYE TAMBWE AFUNGUKA UJIO WA CHIRWA YANGA

Mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe amesema kucheza timu kubwa kama Yanga kunahitaji ujasiri kutokana na usajili unaofanywa kila wakati.

Ujio wa mshambuliaji mpya kwenye kikosi cha Yanga, Mzambia Obrey Chirwa, unaonekana kutishia maisha ya Tambwe kwenye kikosi cha kocha Hans Pluijm, lakini mwenyewe amesema haitakuwa rahisi kama ambavyo watu wanadhani, kwani ataendelea kucheka na nyavu kama kawaida.

“Nitapambana uwanjani na kocha ndiye atakuwa na maamuzi, lakini nakubali Chirwa ni mchezaji mzuri ana uwezo mkubwa wa kumiliki mpira na bado kijana, tusubiri kuona,” alisema Tambwe.

Aidha Tambwe alisema anabahati kubwa na klabu ya Yanga hivyo anaamini ataendelea kufanya vizuri zaidi katika safu ya Ushambuliaji ya Yanga.

Tayari Paul Nonga ameshaomba kuondoka klabuni hapo kutokana na kukosa nafasi ya kucheza na kutaka kwenda kujaribu sehemu nyingine.

Bonyeza Hapa Ku-Like Ukurasa Wa Soka24 Facebook

0 comments:

Post a Comment