Messi amefikia maamuzi hayo baada ya Argentina kukubali kipigo katika mechi ya fainali ya Copa America 2016 huku yeye akikosa mkwaju wa penati.
Messi alikosa penati katika fainali hiyo baada ya dakika 120 kumalizika huku timu zote zikiwa hazijafungana na kufika hatua ya mikwaju ya penati ambapo Chile iliitandika Argentina jumla ya mikwaju 4 - 2.
"Ni ngumu sana, lakini nimeshafikia maamuzi. Sasa hivi sitajaribu tena na sitarudi tena nyuma, Nimejaribu mara nyingi kutafuta taji lakini nimefeli" alisema Messi.
Messi alipiga mpira juu na mbali kabisa na lango huku Claudio Bravo akiokoa mkwaju uliopigwa na Biglia na kumwacha Francisco Silva akifunga goli la ushindi kwa upande wa Chile na kuwapata taji la pili la Copa America.
Ukiachana na uhaba wa mataji katika kikosi chake cha timu ya taifa, kwa upande wa klabu yake ya Barcelona Messi amepata mafanikio makubwa kwa kufanikiwa kutwaa kombe la klabu bingwa ulaya mara nne, ligi kuu Hispania (La Liga) mara 8 na Copa del Rey mara 4.
0 comments:
Post a Comment