Rage amesema Sheria ya Usajili ya michuano ya Kombe la shirikisho namba 4 na 5 inaonyesha kuwa wachezaji hao hawaruhusiwa kucheza kama hawajapewa leseni na kamati ya sheria na usajili ya shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Rage aliwataja wachezaji hao kuwa ni Hassan Kessy, Juma Mahadhi, Ben Kakolanya na Vicent Andrew.
"Kwa Mujibu wa sheria hizo za shirikisho la Soka Afrika (CAF) suala la usajili lina sehemu mbili. Wachezaji wanatakiwa kusajiliwa kabla ya januari 15 au kabla ya Agosti 10 ndipo waruhusiwe" alisema Rage.
Akifafanua zaidi suala hilo Rage amesema Yanga baada ya kufuzu michuano hiyo mapema,TFF kama ilikuwa inataka kuwasaidia Yanga, rais wake ambaye ni Jamal Malinzi alitakiwa kuitisha kikao cha dharula kufanya marekebisho ya kanuni za usajili kuisaidia timu hiyo kupata leseni za wachezaji hao. Kwa vile walishindwa kufanya hivyo sheria zinaeleza kuwa ili wachezaji hao waruhusiwe kucheza ni lazima wapitishwe na kamati hiyo ya TFF.
Aidha Rage aliongeza kuwa kamati hiyo haijakaa kwani utaratibu wao uliopo ni hadi kusubiri dirisha la usajili lifungwe kisha ikae na kupitia majina ambayo hayana pingamizi na ndipo iwaruhusu wachezaji hao kuitumikia klabu yao mpya.
Aliyewahi kuwa makamu wa rais chini ya Uongozi wa Leodegar Tenga mwaka 2004 naye alisema "Ni lazima Yanga wawe makini kwenye hilo wasipoangalia inaweza kuwagharimu"
Hata hivyo habari zinasema kuwa TFF imeshampa leseni Kessy inayomwezesha kucheza katika mchezo wa leo dhidi ya Mazembe.
0 comments:
Post a Comment