Tuesday, June 28, 2016

RASMI:DANI ALVES ATUA JUVENTUS

Mchezaji wa kimataifa wa Brazil, Dani Alves ametua katika klabu ya Juventus akitokea Barcelona.

Dani Alves amekamilisha uhamisho wake wa kujiunga na Juventus akitokea Barcelona na kusaini mkataba wa miaka miwili na mabingwa hao wa Serie A.

Beki huyo wa kulia ameondoka Camp Nou akiwa mchezaji huru baada ya kuitumikia Barcelona kwa muda wa miaka 8 alipojiunga akitokea Sevilla kwa uhamisho Euro milioni 30.

Like Ukurasa Wa Soka24 Facebook Hapa


0 comments:

Post a Comment