Hodgson 68 amekuwa kocha wa Uingereza kwa muda wa miaka minne baada ya kuchukua nafasi ya Fabio Capello na amefanikiwa kushinda mechi 3 tu kati ya 11 alizoshiriki katika fainali za michuano mbalimbali.
Iceland yenye idadi ya watu 330,000 ilikuwa ni miongoni mwa timu ambazo hazikupewa nafasi ya kufanya vizuri katika michuano hiyo.
"Sasa ni muda wa mtu mwingine kuangalia maendeleo ya kundi la wachezaji wenye njaa ya ubingwa na vipaji vikubwa" alisema Hodgson.
"Wamefanya kazi kubwa na kila nilichowaambia wafanye. Ni matumaini yangu kuwa mutaendelea kuiona Uingereza katika fainali za michuano mikubwa zaidi hivi karibuni" aliongeza kocha huyo ambaye amefanikiwa kushinda mechi 33 tu kati ya mechi 56 ambazo Uingereza imecheza yeye akiwa kocha mkuu.
Wanaodhaniwa kuchukua mikoba ya Hodgson ni kocha wa timu ya vijana ya Uingereza chini ya umri wa miaka 21 aliyekuwa kocha wa zamani wa Middlesbrough Gareth Southgate, Wengine ni Gary Neville, Meneja wa Crystal Palace Alan Pardew, Meneja wa Bournemouth Eddie Howe na kocha mpya wa Celtic Brendan Rodgers, Arsene Wenger pamoja na Jose Mourinho wote wanahusishwa kurithi mikoba ya Roy Hodgson.
0 comments:
Post a Comment