Walter Musona |
Yanga inakaribia kuinasa saini ya mshambuliaji hatari kutoka nchini Zimbabwe, Walter Musona ambaye anamudu kucheza nafasi ya Tambwe.
Kwa upande wake Tambwe amesema hana hofu yoyote ya kupoteza namba katika kikosi cha kwanza Yanga lakini akikiri kuwa soka ni mchezo wa ushindani hivyo kujituma kwake ndo kutamhakikishia nafasi klabu hapo.
Tambwe |
"Nawakaribisha wachezaji wapya kwa ajili ya kuipigania Yanga, lakini hitakuwa rahisi kupoteza nafasi yangu." aliongeza.
Tambwe alijiunga na Yanga akitokea Simba na amekuwa na uzoefu mkubwa katika ligi kuu Vodacom huku akifanikiwa kutwaa tuzo ya mfungaji bora wa ligi hiyo msimu huu kwa kufikisha jumla ya magoli 21 katika ligi.
==============
Bonyeza hapa ku-Like Page yetu ya Facebook
==============
0 comments:
Post a Comment